Vigezo na Masharti
Kwa kununua kwenye tovuti hii unakubaliana na masharti yafuatayo.
1. Bei
Bei zote zimeandikwa kwa Shilingi ya Tanzania (TZS) na zinaweza kubadilika kulingana na soko. Bei inayoonekana wakati wa malipo ndiyo halali.
2. Malipo
Malipo hufanyika kwa mtandao wa simu (M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money, Halopesa) kupitia Abliner. Oda inathibitishwa tu baada ya malipo kukamilika.
3. Usafirishaji
Dodoma: siku ile ile au siku inayofuata. Mikoa mingine: siku 1–3 za kazi kupitia kampuni za usafirishaji. Gharama za mikoa ya mbali zinaweza kuongezeka na utaarifiwa kwa simu.
4. Dhamana
Laptop na desktop zina dhamana ya miezi 3 hadi 12 kutegemea bidhaa. Chaja zina dhamana ya miezi 3. Dhamana haihusishi uharibifu wa maji, kuanguka au kuchezewa na fundi mwingine.
5. Kurudisha bidhaa
Bidhaa yenye hitilafu ya kiwandani inaweza kurudishwa ndani ya siku 7 ikiwa na risiti na vifungashio vyake.
6. Mawasiliano
WENAC TECHNOLOGIES, Nyerere Road, Dodoma, Tanzania. Simu: 0770290751.